UMASIKINI WACHANGIA ONGEZEKO LA UTAPIAMLO NCHINI

Kudorora kwa uchumi na kukosa elimu sahihi ya lishe bora kwa jamii kumechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa utapiamlo kwa jamii.

Idadi ya watoto wanaopoteza maisha kutoka na ugonjwa huu imefikia watoto 130 kila siku kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012.

Idadi hii ambayo inahofiwa kuongezeka kila kukicha inakuja huku Tanzania hapo kesho itaungana na nchi zingine duniani katika kuadhimisha siku ya utapiamlo Duniani.

Kasi ya kukua kwa kiwango cha umasikini miongoni mwa watanzania kumeendelea kuwa chanzo kikubwa cha ongezeko la ugonjwa wa utapiamlo nchini.

Asilimia 42 ya watoto wa Tanzania chini ya umri wa miaka 18 wana utapiamlo huku idadi hii ikihofiwa kuongezeka.

Kwa mujibu wa daktari wa wodi ya watoto wanaougua utapiamlo katika hospitali ya rufaa bugando jijini Mwanza dakta Julieth Kibirigi,tatizo la ugonjwa huo linachangiwa na kutozingatia mlo kamili kwa watoto.

Katika wodi hii watoto watano hadi saba hupokelewa kila siku wakiwa na tatizo la ugonjwa huu.

Jitahada zinazofanyika hapa nikuhakikisha watoto wanapata tiba kamili ya ugonjwa huu lakini pamoja na jitihada hizi bado kuna changamoto kadha wa kadha. 

Katika kipindi cha miaka 5 zaidi ya watoto laki mbili na elfu thelathini na nne walipoteza maisha kutoka na ugonjwa huu nchini

Tanzania, sababu zingine ambazo ni chanzo la ongezeko la ugonjwa ni pamoja na Bajeti ya afya kidogo ya serikali, upungufu wa vitamini na madini kwa kina mama wajawzito,huduma duni ya afya kwa watoto wachanga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo