RASIMU YA KATIBA MPYA, RAIS KUSHTAKIWA MAHAKAMANI

Jaji Joseph Sinde Warioba Akizindua Rasmu ya Katiba Mpya Leo jijini Dar es Salaam
Dar es Salaam, Tanzania. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hivi punde kwamba katika Rasimu ya Katiba kwa ajili kutengeneza Katiba Mpya ijayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imependekeza kwamba matokeo ya rais yahojiwe mahakamani.

Kwa lugha nyingine ni kwamba katiba ijayo itarusu rais kushtakiwa mahakamani endapo matokeo yake yatatiliwa shaka na wagombea wengine. Jaji Warioba ameyasema hayo hivi punde wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya katika tukio la kihistoria nchini Tanzania.

"Imependekezwa kwamba matokeo ya rais yatahijiwa mahakamani lakini kwa masharti," amesema Jaji Warioba hivi punde.

Jaji Warioba ametaja masharti hayo ni kwamba wagombea wa urais ndio watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo. Pili, matokeo hayo yanatakiwa kuhojiwa ndani ya mwezi mmoja tu na si vinginevyo.

Amesema pia tume imependekeza kuwapo kwa wabunge wa aina mbili ambao ni wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wengine wa kuteuliwa na rais. Pia amesema kwamba kutakuwapo kwa utaratibu wa wanawake kugombea katika majimbo. Kwa maana hiyo hakutakuwapo kwa wabunge wa Viti Maalumu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo