Kikosi cha zima moto mkoani iringa kimefanya ziara katika vyuo na
shule za bweni lengo likiwa ni kutoa elimu ya tahadhari ya kinga ya moto na
namna ya kujikinga punde majanga yatokeapo.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari hizi,Kamanda mkuu wa kikosi cha zima moto Kenedy Komba, amesema kuwa
katika ziara hiyo amebaini kuwa shule nyingi hazina vifaa na nyingine kuwa
navyo vichache na amewapa siku 14 ya kuwa na vifaa hivyo.
Komba
amesema kuwa wazazi wanapaswa pale tu wanapowapeleka watoto wao mashulen ni
vyema kuuliza juu ya usalama wa shule katika majanga na hata vyeti vya
tahadhali ya kinga na moto.
Aidha
ametembelea shule na vyuo 12 zilizopo ndani na nje ya manispaa ya iringa.