MAITI 30 ZAPATIKANA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR

 
Jengo hilo lilikuwa na ghorofa zaidi ya zilizoruhusiwa

Maafisa wa polisi hapa nchini wanasema kuwa takriban maiti thelathini wamepatikana kutoka kwa vifusi vya jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam Ijumaa.

Hadi sasa watu kumi na saba pekee ndio wamepatikana wakiwa hai katima jengo hilo.

Wengine wengi bado hawajapatikana. Wengi wa waliouawa walikuwa wapita njia au wajenzi.

Watoto waliokuwa katika uwanja wa kuchezea uliopakana na jengo hilo, walikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Polisi wanasema kuwa wamewakamata watu wanne baada ya rais Jakaya Kikwete kutembelea eneo la janga na kuwataka maafisa wa utawala kuwachukulia hatua waliohusika na ujenzi huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo