IRINGA YAKUMBWA NA MAAFA YA MVUA

Mtoto aliyenusurika kifo 
Mfereji  unaotiririsha maji na  kusababisha nyumba hiyo kubomoka
Mwenye nyumba  hiyo akionyesha mfereji unaomwaga maji juu ya nyumba yake
Wananchi pamoja na viongozi  wa mtaa Mabida  Mlandege  mjini Iringa leo




 


Tukio  hilo  limetokea  majira ya  saa 4 usiku  wa kuamkia  leo ambapo chanzo cha kuporomoka kwa  chumba  hicho  kinatajwa kwa  ni mvua na maji  yanayotiririshwa na mmoja kati ya  majirani  wa eneo hilo ambae amejenga  juu ya mlima .

Wakizungumza na mtandao huu  mmiliki wa nyumba hiyo Grace Mlela alisema  kuwa   wakati  tukio  hilo  likitokea  ndani ya chumba  hicho alikuwepo mtoto  wa  miaka miwili ambae  aliokolewa  baada ya  nyumba  hiyo kuanguka .

hata  hivyo  alisema mbali ya  kuwa  chanzo ni mvua ila utiririshaji maji  ovyo unaofanywa na mmoja kati ya  wamiliki  wa nyumba  za  jirani eneo hilo ni chanzo cha nyumba  hiyo kuanguka.

Mlale  amesema kuwa kutokana na tukio  la kutiririsha maji  ovyo  wamepata  kulalamika  ofisi ya  serikali ya mtaa ila hakuna  hatua  zinazochukuliwa  dhidi ya mhusika.

Mwenyekiti  wa  serikali ya mtaa huyo Bi. Desdelia Chahe na balozi  wake Lucy  Kilosa wamefika  eneo hilo na  kuthibitisha  kutokea kwa tukio  hilo na kuwa  kwa  sasa  wanajiandaa kumwita  mhusika  wa utiririshaji maji ovyo  ili  kufikishwa  mbele ya sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo