DKT BILAL, ASHIRIKI SHUGHULI ZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU ERNEST MWIPOPO KARIMJEE DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo April 5, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji ndugu wa marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo April 5, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho.
 Mmoja wa majaji akibeba picha ya marehemu wakati majaji hao wakishuha jeneza hilo lenye mwili wa marehemu, ili kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee leo. Picha na OMR
 Majaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, wakishusha katika gari kwa ajili ya kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee, leo
 Majaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, wakishusha katika gari kwa ajili ya kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee, leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee leo kushiriki kwenye shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga mwili.Picha na OMR


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo