UBOVU WA BARABARA MAKETE WAMCHEFUA DC

Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro

Mkuu wa wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro amewataka wananchi  wa Makete  kushiriki katika  ukarabati wa miundombinu ya barabara pindi tatizo linapotokea hasa maeneo korofi
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu kwa njia ya simu Bi.Matiro alisema wananchi wanatakiwa kuwa na ushirikiano pindi barabara zinapokuwa zimeharibika ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Makete 

Hata hivyo alisema kuwa viongozi wa Tanrods mkoa
   wa Njombe wameshapewa taarifa kuhusiana na tatizo hilo lililoko katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo hasa katika kijiji cha Ivalalila ambapo magari ya kutoka Mbeya kuja Makete yanashindwa kupita kulingana na ubovu wa barabara hiyo

Mtandao huu ulifika eneo la tukio nakujionea hali halisi  ya barabara ambapo mpaka sasa hakuna mawasiliano kutoka Makete kwenda jijini Mbeya kupitia Ivalalila kutokana na shimo lililopo eneo la Ivalalila.
 
Mtandao huu haukiishia hapo ulikwenda moja kwa moja kuongea na wamiliki wa vyombo vya usari ambapo mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Japanise, Junich Daniel alimarufu kama  Mwarabu alisema "kwa hali hii inakoelekea usafiri wa Makete na Mbeya hautakuwepo kutokana na tunaingia gharama nyingi kufanya marekebisho ya magari kutokana na mara nyingi kugongesha katika mashimo ya barabarani"
Akiendelea Mwarabu alisema"natumia fursa hii kumuomba mbunge na uongozi mzima bila kumsahau waziri mwenye dhamana ya ujenzi kuweza kutufanyia marekebisho katika barabara za wilaya ya Makete kuwa hali tete hususani nyakati za masika 

Na Riziki Mgaya,Makete


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo