Wakati serikali ikisisitiza wajasiriamali kujiunga katika vikundi ili
kurahisisha kupata mikopo, Benki ya NMB Tawi la Mkwawa mkoani Iringa
limedaiwa kuwa na ubaguzi kwa wafanyabiashara wakati wa utoaji wa
mikopo.
Wakizungumza katika semina iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa
wanachama wa NMB Business Club iliyofanyika katika Ukumbi wa chuo Kikuu
Huria mkoani Iringa, wamesema Benki benki hiyo inaendelea kupoteza hadhi
yake kutokana na kutoa mikopo kwa upendeleo na kuwatelekeza bila sababu
baadhi ya wafanyabiashara wenye vigezo vyote kwa kushindwa kupata
mikopo.
Wamesema mara nyingi wamekua wakipata pungufu ya kiasi cha mkopo
walichokiomba bila maelezo yakujitosheleza yanayoonesha biashara zao
hazijatimiza vigezo vya kupata fedha walizoomba.
Wameongeza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanapatiwa fedha nyingi
zaidi ya shilingi milioni mia wakati katika maombi yao na miradi
waliyonayo hawastahili hata kupatiwa milioni 10 hali ambayo inawafanya
wafanyabiashara hao kuitilia mashaka Benki hiyo.
Akijibu tuhuma hizo
Dickson Pangamawe kutoka kitengo cha mikopo cha Benki ya NMB makao
Makuu, amesema kuwa atahakikisha anafuatilia malalamiko ya
wafanyabiashara hao ili kubaini sababu ya kupewa mkopo pungufu