Na
Magreth Kinabo-Maelezo
WAZIRI
wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amezitaka Mamlaka zinazosimamia Usambazaji
wa maji safi na maji taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO na
DAWASA) kuhakikisha tatizo la wizi wa maji
linatafutiwa ufumbuzi, huku akionya kuwa mfanyakazi
atakayehusika atafukuzwa kazi.
Akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hizo Dar es Salaam Jana Prof.Maghembe amesema jumla ya maji lita mil 300 yaliitajika kusambazwa lakini kutoka katika vyanzo vikuu vya maji lakini kutokana na kuwepo kwa utaratibu mbovu inasababisha asilimia 56 ya kupotea ambapo kati ya hizo asilimia 30 yanaibwa na kudai kuwa wanawajua na kuwafahamu wezi hao.
Amesema mbali na uchakavu wa miundombinu inayosababisha maji kupotea pia alizitaja sababu nyingine ni mgawo wa upelendeleo unafanywa na baadhi ya viongozi katika kusimamia maji hayo ili waweze kujipatia chochote.
Prof.Maghembe
amewataka maofisa wanaosimamia mgawo wa maji kuacha kudanga watu kwa
kuwapa maji kwa masaa machache wakati ni haki yao kwa siku hiyo kupata maji
kama utaratibu ulivyo.
"Nataka muwe wazalendo katika kuwatendea haki wananchi kwa kuwapa maji badala ya kuwasambazia rafiki zenu wauza maji ili mpate mshiko,nikigundua kuna sehemu maji hayakupelekwa meneja husika na wafanyakazi wake nitawafukuza kazi papo hapo"alisema.
Alidai
kuwa baadhi ya wafanyazi wakishirikiana na wauza maji kwa kuwafungia mitambo
akitolea mfano katika eneo la Mkwajuni ambapo kuna mfanyabiashara ambaye
anasambaza maji hadi katika maeneo ya Mwanyamala ingawaje mitambo hiyo
ilishaondolewa ila cha kushangaza hadi juzi imefungwa tena.
"Bomba
hilo la Mkwajuni ni kubwa mtu wa kawaida hawezi kufunga mitambo hiyo hata hivyo
kuna mitambo kumi katika maeneo hayo ambayo nayo inaiba maji"alisema
Prof.Maghembe
alisema kutokana na mazingira hayo kwa namna moja nyingine mnahusika kwa
kuhujumu maji hivyo hatuwezi kukubali tabia hiyo.
"Sikubali
kuona wafanyakazi ambao wanahujumu mashirika nitawachukulia hatua
wale wote watakaokamatwa pamoja na kuwafukuza kazi mara moja "alisema Prof
Maghembe.
Prof
Maghembe aliwataka Wenyeviti wa mashirika hayo kuhakikisha kuwa watu wote
wanauza maji na malori wajiandikishe na kutambuliwa kisheria na
DAWASCO, maji wanayoyauza yawe safi, wawe na mita , leseni , namba ya
mplipa kodi , pia bei ya kuuza maji idhibitiwe na EWURA .
Alitaka
zoezi hili lianze kuanzia Mwezi Machi hadi April 30, mwaka huu
liwe limekamilika.
"Hivyo nataka wizi wa maji ifikie asilimia zero mara moja kwani hatuwezi kubadilisha maisha yenu wakati maji yanapotea. Ninyi mabwana maji acheni vituko haiwezekani mnafanya mambo haya mpewe heshima ya kuwahudumia Watanzania."alisisitiza Prof Maghembe.
Aliwaomba
wananchi na wafanyakazi wengine kuwataja wezi kwani atakayetaja atalipwa
sh.100,000 na atalindwa.