Diwani Omary
Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na
wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua
Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za
diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa
kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
Wasanii wa
filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B', Vicent Kigosi 'Ray', Irene
Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo
kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa
vijana wa Kata hiyo.
Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzinduzi huo
KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo wakati wa uzinduzi huo
Treka likionesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
KITUKO:
Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake
kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la
wazee, kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za
uzinduzi huo shambani
J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
BAADAYE:
Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo
walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili
kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
Diwani
Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji
vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini
Kariati akioneshwa maeneo yaliyoathirika
Wazee wakiomba
dua ya kheri baada ya shughuli za uzinduzi wa Kampeni ya kilimo kwanza
na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha zote na Bashir
Nkoromo wa Daily Nkoromo Blog
















