Katibu wa CCM wilaya ya Makete Bw. Miraji Mtaturu
Chama
cha mapinduzi CCM wilayani Makete kimetoa mpango kazi wa mambo
watakayoyatekeleza kwa mwaka 2013 ikiwa ni pamoja na kuisimamia serikali
kutekeleza ipasavyo miradi ya maendeleo
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa CCM wilayani Makete Bw. Miraji
Mtaturu amesema mwaka 2013 ni mwaka wa kazi kwa chama hicho kuzidi kufanya kazi
ikiwemo kuibana serikali pale inapozembea
Amesema
kwa hivi sasa wanakwenda katika matawi yote ya chama hicho ndani ya Makete ili
kuzungumza na viongozi wote wa CCM kwenye matawi kuwaagiza kuwasimamia viongozi
wa serikali ili wafanye kazi kama serikali inavyotaka ili kuondoa uzembe
unaoonekana kwa baadhi ya watendaji wa serikali
“Kikubwa
ni kuisimamia serikali ili miradi mbalimbali itekelezwe na kwa maana hiyo
tutakwenda kukutana na viongozi wote wa CCM kwenye matawi yote ili tuwaelekeze
namna ya kuibana serikali kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali” alisema Mtaturu
Ameitaja
baadhi ya miradi hiyo kuwa nia pamoja na miundombinu ikiwemo barabara, ujenzi
wa madarasa, zahanati pamoja na miradi ya kilimo
Katika
hatua nyingine katibu huyo amezungumzia maandalizi ya maadhimisho ya miaka 36
tangu kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ambapo maadhimisho hayo kimkoa
yanatarajiwa kufanyika katika wilaya ya Makete katika kata ya Tandala
Amesema
maandalizi hayo yanakwenda vizuri na maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika
Februari 5 na yataongozwa na kiongozi wa kitaifa wa chama hicho, ambapo
kutakuwa na maandamano yatakayoanzia kwenye ofisi za CCM kata ya Tandala hadi
viwanja vya chuo cha ualimu Tandala na baadaye kuwa na mkutano wa hadhara
katika viwanja vya chuo hicho
Mara
baada ya mkutano huo wa hadhara jioni kutakuwa na mpira wa miguu ikifuatiwa na
mdahalo wa kubadilishana mawazo utakaofanyika katika ukumbi wa chuo hicho
“Niwatie
shime viongozi na watu wote mfike hapo chuoni Tandala kwenye mdahalo huo wa
kujadili masuala mbalimbali ili kuongeza ujuzi wa mambo yanayotuzunguka”
alisema Mtaturu
