Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Mbeya Martin Joseph leo amekabidhiwa mpira wa miguu kutoka shirika la utangazi la Uingeleza na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mbeya (Mbeya PRESS klabu) Christopher Nyenyembe baada ya kuibuka mshindi kwa kutabili mchezo kati ya Chelsea na Aston Villa.
Zawadi hiyo alikabidhiwa leo na mwenyekiti huyo katika ofisi za gazeti za la Tanzanzania Daima katikati ya jiji la Mbeya kutoka shirika la utangazaji la Uingeleza BBC kati ya Chelsea na Aston Vila ikiwa ni ligi kuu nchini humo maarufu kama ya Barclys preamer leage ambapo Joseph alitabili timu ya Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 4-2 .
Akiongea na mbele ya waandishi wa Habari mshindi huyo amesema kuwa yeye kama mshabiki wa timu ya Chelsea alimua kucheza bahati nasibu hiyo kwa kuwa alikuwa ana imani na kikosi cha timu yake licha ya kuwa siku za hivi karibuni timu hiyo imekuwa ikisuasua katika ligi ya England.
Alisema taarifa za ushindi wake alipewa na mwandishi na mtangazji wa kipindi cha michezo cha radio 5 fm ya mjini Arusha Willy Cosmas baada ya siku moja kufanyika kwa mpambano huo.
Radio 5 fm ni moja ya radio zinashirikiana na shirika la utangazaji la Uingeleza BBC kurusha matangazo ya ligi kuu ya Uingeleza chini Tanzania
‘Iilikuwa mida ya jioni kama saa mbili hivi nikiwa nyumbani nimelala simu yangu ikiita mara tuu baada ya kupokea niliulizwa maswali ambayo kwangu yalinipa hofu lakini baadaye nilipo ambiwa mimi ndiye ,mshindi wa bahati nasibu hiyo kwa kweli sikulala kabisa na hata hivi nilikuwa naona siku hazisogei lakini furaha yangu imetimia zaidi hasa nilivyo kabidhiwa mpira’ Alisema Martin aliye ambatana na nahodha wa timu yake ya vijana ya mtaa wa Isanga ya Gusagusa Star Lusajo Majaliwa
Katika hatua nyingine mshindi huyo anaye tokea mitaa ya Jakaranda jijin hapa aliwasii mashabiki wa timu ya Chelsea kuwa na imani na timu yao na pia wawe na imani na bahati nasinbu hiyo kuwa ni ya kweli na sii changa la macho.
Mchezo wa timu ya Chelsea na Aston Villa ulipigwa majuma mawili yaliyo pita huku timu ya Chelsea ikibuka na ushindi mnono katika uwanja wa Ugenini.
Akikabidhi zawadi hiyo Mwekiti wa Mbeya Press Klabu amesema mshindi huyo kwamba mpira aliopata iwe chachu kwake ya kujituma katika mchezo huo na kuweza kuwa mchezaji bora wa siku za usoni kwani ana nafasi kubwa ya kuweza kuwa mchezaji bora kutokana na umri wake kuwa mdogo.
‘Kwanza nakupongeza kwa kuwa mshindi peekee kutoka mkoni kweti kati wa washindi 6 kutoka Tanzania kitu cha msingi nikuombe usiuze mpira huu bali uhutumie kwa ajilki ya manufaa yako na jamii inayo kuzunguka ilin=muweze kiuibua vipaji vipya’ alisema Nyenyembe.
Alisema kuwa mpira kwa sasa ni kazi na Ajira kwa hiyo ana kila sababu za kujitiuma ili kuwa mchezaji muhimu kwa taifa bila kusaau masomo.
Naye naodha wa timu Gusagusa Star Lusajo Majaliwa alipongeza hatua ya mchezaji kwake kuwa moyo ya kujituma katika bahati nasibu kwani watu wengi wamekuwa wakikata tama na kwamba mpoira huo umekuja muda mwafaka kwa timu yao kwani muda mrefu wamekuwa na tatizo la mpira.