Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu hapa nchini marehemu Steven Kanumba amesema maziko ya mwanaye yatafanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne 10/04/2012
Akizungumza na mtandao huu Mama Kanumba amesema ndugu wengi wa marehemu Kanumba wapo jijini DSM hivyo akaona ni vyema azikwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
Kabla ya maziko hayo ibaada ya kumwombea marehemu Kanumba itafanyika katika viwanja vya Leaders ambapo pia watatoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu