WANAFUNZI WEZI..........


                            Mkuu wa shule ya Iwawa Sekondari Isdori Ngimba

Imebainika kwamba wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete wanaodaiwa kuiba hand lens moja wakati wa mtihani wao wa mwisho wa kumaliza kidato cha nne katika somo la biolojia mwaka jana wametakiwa kuhakikisha wanalipa gharama au kuirudisha ili waweze kuchukua vyeti vyao

Akizungumza wanahabari mkuu wa shule hiyo Isdori Ngimba amesema kuwatoza wanafunzi hao kiasi cha shilingi 10,000/- kila mwanafunzi na bila kumpa risiti ya fedha aliyotoa siyo kuwakomoa wazazi bali ni kutoa fundisho wanafunzi wengine ili nao wasije wakafanya hivyo

Amesema gharama ya hand lens hiyo iliyopotea ni shs.7,500/= hivyo kutokana na gharama za ufuatiliaji wa kwenda kununua kila mwanafunzi atatakiwa kulipa shilingi 10,000/=



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo