
Taharifa kutoka kuko New Jersey Nchini Marekani zimasema Nguli wa muziki Duniani Mwanamama Whitney Houston Aliyefariki mwishishoni mwa wiki anatarajiwa kuzikwa kesho Feb 18 katika eneo lenye uwezo wa kuchukua watu 18,000.
Mwili wa Marehemu Whitney ulisafirishwa juzi usiku kwa ndege ya kukodi kutoka Los Angeles hadi New Jersey ambako ameifadhiwa katika mochwari ya Newark mahali ambako maziko ya baba yake,John Russell Houston Jr.yalifanyika mwaka 2003.
Taharifa zinasema kifo cha Whitney yawezekana kimetokana na kula chakula kilichochanganywa na dawa za kulevya na wakati huo huo alitumia pombe..
Vile vile wanae wa kike ambaye alitishia kujiua mara baada ya kupata taharifa ya kifo cha mama yake ,Hivi sasa anaeendelea vyema mara baada ya kulazwa katika Hospital moja nchini humo..
Na Pro24