BAADA ya Christina Milian kuachwa



MIAMI, MAREKANI
BAADA ya Christina Milian kuachwa na mumewe aitwaye The Dream, dada huyo amerudi kwa aliyewahi kuwa mpenzi wake wa muda mfupi, rapa Lil Wayne na anatarajia kufanya kazi chini ya lebo ya kaka huyo ya Young Money.

Ni takribani miaka sita imepita tangu mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa Dip it Low na Say I, aachie albamu ya kwanza.

Milian anasema alimpelekea nyimbo zake Wayne, alipozisikiliza alizipenda na kukubali kufanya naye kazi chini ya lebo hiyo ambayo ina mastaa kama Nick Minaj, Tyga, Drake, Jay Sean, Bird Man n.k.

Christina Milian aliachia albamu ya mwisho ya 'So Amazin' mwaka 2006.
Akiwa na Young Money anatarajia kuachia albamu itakayoingia sokoni katikati ya mwaka huu.

(Na Mwanaspoti)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo