Mashabiki Simba wapiga harambee kununua basi


Jumla ya kiasi cha Sh 42.4 milioni zimechangwa katika harambee maalumu ya kununua gari aina ya Coaster ambalo litasaidia mashabiki na wanachama  wa Simba  tawi la Mafinga wilayani ya Mufindi, mkoani Iringa kwa ajili ya safari zao kuisapoti timu yao pindi itakapokuwa ikicheza.


Hayo yamebainishwa leo Jumatatu, Desemab 19, 2022 na Mwenyekiti wa tawi la Simba Mafinga, Dickson Mtevele ( maarufu Villa) wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo ambapo amesema wanawashukuru wanasimba kwa kujitokeza kwa wengi kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo.

Aidha  Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika harambee hiyo walilenga kukusanya kiasi cha Sh 62.9 milioni ambazo zinahitajika lakini hadi sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh42.4 milioni kwa ajili ya kukamilisha ununuzi wa basi hilo.

"Kama Mungu akitusaidia kufanikisha jambo letu ya ununuzi wa basi tutafurahi sana kwa sababu  tayari tumeulizia gharama ya basi hilo kuwa ni Sh62.9 milioni lakini hadi sasa tumefikia asilimia 95 ya harambee yetu hivyo inatupa moyo kuwa jambo letu litafanikiwa," amesema Mtevele

Pia Mtevele amesema kuwa kupatikana kwa basi hilo litakuwa msaada mkubwa kwao mbali na kutumiwa na  mashabiki na wanachama kwa ajili ya kwenda kuisapoti timu yao lakini pia watalitimia kama chanzo cha  kuwaingizia mapato katika tawi lao.

Pia Mtevele amesema mbali na ununuzi wa basi hilo lakini mipango yao kama Tawi  ni kuongeza idadi ya wanachama ambapo katika harambee wamepata  zaidi ya Mashabiki na wanacha 500 wameweza kuhudhulia katika hafla hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo