TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi
Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa
uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2012