Shamba Boy Awapachika Mimba Mabinti Watatu wa Tajiri Wake


Shamba boy Mkenya ameweka historia ya kuwapachika mimba mabinti watatu wa tajiri wake.


Akishiri kisa hicho kwenye mtandao wa Facebook, Mbunge wa zamani, Seneta Shehu Sani alifichua kuwa warembo hao watatu wana wazazi wakali ambao kwa kawaida waliwafungia ndani ya nyumba na kuwanyima nafasi ya kutangamana na marafiki.


Inaripotiwa kwamba mfanyakazi hyo pekee ndiye aliyekuwa akitangamana nao. Kama ilivyoelezwa kwenye chapisho hilo, shamba boy huyo alianza kujamiana na dada wote watatu bila wazazi wao ambao ni Wakristo wenye itikadi kali kujua.


Tovuti ya tuko imetambua kwamba mfanyakazi huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzaliwa wa pili na alikamatwa katika tendo hilo na dada yake mkubwa. Wakati huo huo, ili kifungua mimba aweze kuweka siri hiyo, alimwomba shamba boy huyo kutosheleza kiu yake ya ngono. Wakiwa wanarushana roho, mzaliwa wa tatu naye aliwafumania katika kitendo hicho na pia alidai hamu yake ya mapenzi ili kujiridhisha ikiwa hawataki awaambie wazazi wao wakali.


Matokeo ya uhusiano wao na mfanyakazi huyo yaligeuka kuwa ujauzito na wote watatu wamejifungua. Baada ya kusikia habari hizo, wazazi hao walipigwa na butwaa kutokana na jinsi mambo yalivyobadilika licha ya jitihada zote za kuwaepusha kutangamana na wanaume. Walipoulizwa ni nani aliyehusika na ujauzito huo, walimwaga mtama na kumtaja shamba boy huyo, habari ambazo zilimfanya mama yao kuanguka chini na kuzirai papo hapo.


Wazazi hao sasa wamekubali matokeo baada ya kupewa ushauri nasaha na kujilaumu kwa kuwa wakali sana kwa binti zao.


Shamba boy naye alipigwa kalamu lakini dada hao bado humtumia pesa na kumpenda kama baba wa binti zao wawili na mtoto wa kiume. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo