Waliolima shamba la Serikali wapewa siku saba kujisalimisha

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanja ameagiza Wananchi waliolima shamba la Serikali la Basotu bila kulipia fedha ya ukodishaji Halmashauri ya Wilaya ya Hanang pamoja na waliojiongezea maeneo kuhakikisha wanalipia ndani ya siku 7 na endapo watakiuka hatua zitaanza kuchukuliwa.


Amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU wa Wilaya ya Hanang Bw Samson Sana kuwahoji wote waliolima bila kulipia kujua mamlaka hiyo wameyapata wapi, ikiwa ni pamoja na kuliagiza Jeshi la Polisi kulinda eneo hilo, kuhakikisha hakuna mwananchi anavuna mazao bila kuonyesha risiti ya kulipia shamba inayoendana na ukubwa halisia wa shamba.

Hata hivyo Bi Janeth Mayanja amewaambia Wananchi waliolima bila kulipia fedha ya ukodishaji wasipolipia mashamba mazao hayo yatataifishwa. •


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo