WATOTO WAISHITAKI SERIKALI BAADA YA BABA YAO KUPOTEA KWENYE NDEGE

Watoto wawili wa kiume wameishtaki Serikali na shirika la ndege la Malaysia kutokana na kumpoteza baba yao katika ndege ya Malaysia Airlines 370.

Watoto hao Jee Kinson mwenye miaka 13, na Jee Kinland wameorodhesha majina ya shirika hilo la ndege, maafisa wa idara ya usalama wa anga na uhamiaji, na mkuu wa kikosi cha jeshi la anga kuwa wamehusika moja kwa moja na upotevu wa ndege hiyo mwezi Machi 8 mwaka huu.
Lawyer
Mwanasheria wa watoto hao, Arunan Selvaraj (katikati) akizungumza na wandishi wa habari nje ya mahakama.

Baba wa watoto hao alikuwa mmoja wa abiria ndani ya ndege hiyo akitokea Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing China, tangu imepotea zimepita siku 237 na jitihada za kuitafuta bado zinaendelea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo