UMEME WAKATISHA HOTUBA YA RAIS RAWLINGS

WIMBI la kukatika umeme mara kwa mara, jana limeitia aibu Tanzania, baada ya umeme kukatika ghafla wakati Rais mstaafu wa Ghana, Jerry Rawlings, akihutubia mkutano wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola.

Tukio hilo, lilitokea mjini Dar es Saama jana katika Hoteli ya Kimataifa ya Serena, ambapo kulikuwa na ugeni mkubwa wa Wabunge wa Jumuiya hiyo kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Shelisheli.

Mara baada ya kukatika umeme, Rais Rawling alishtuka na kusema …Ow! It’s not me ….but it’s normal, akimaaniasha sio yeye, lakini ni kawaida, kisha akaedelea na hutuba yake, huku akiwa gizani kwa dakika moja na kisha kuhitimisha.

Hali ya giza, iliedelea kwa takribani dakika nne hivi, kisha umeme ukarejea na mambo yakaendelea kuwa kama kawaida.

Katika hotuba yake, Rais Rawling, alisema demokrasia sio adui wa maendeleo ya Afrika, lakini ni kichocheo cha kuzifanya serikali barani, kuzidisha huduma za kijamii kwa wananchi wanaowatawala.

Alisema kuwapo kwa upinzani katika demokrasia, ni njia pekee ya kuimarisha utawala wa kisheria unaozingatia haki za binaadamu na uwajibikaji wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea.

“Utawala wa kidemokrasia ni utamaduni ambao unakuwa polepole, nimekaa katika mfumo wa utawala wa Afrika kwa muda mrefu, kwa hiyo naelewa suala hili kwa undani sana, kweli kwa sasa kunababadiliko makubwa,”alisema Rawlings.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Mmasekgoa Masire-Mwamba, alisema demokrasia inachochea nafasi ya uwakilishi bora wa wanachi katika Serikali.

Naye Mbunge we Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), alisema kutokana na mfumo huo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, halina budi kubadirisha kanuni kwa kuweka kanuni ambazo zitatoa fursa ya kutosha kwa kambi ya upinzani kutoa hoja zilizo na maslahi kwa taifa.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, alisema mkutano huo unalenga kuzisaidia Serikali za Afrika kuimarisha utawala bora na uwajibikaji kwa wananchi.

Chanzo: Mtanzania


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo