Kauli ya Dc Makete Baada ya Msiba wa Maria na Consolata

Wapendwa Mapembelo...

Nawatakia heri na baraka kwa upendo wa Mungu.

Kwa majonzi makubwa tumewapoteza watoto wetu, Maria na Consolata ni imani yangu kuwa Mungu aliwaleta hapa Duniani kwa makusudio yake na amewachukua ktk wakati wake alioupanga yeye, basi hatuna budi kumshukuru kwa matendo yake maku na kumrudishia sifa.!!

Wote tunafahamu kuwa watoto hawa walizaliwa na kulelewa hapa Makete na wazazi wao walikuwa watumishi hapa Halmashauri ingawa kwa mapenzi ya Mungu walishatangulia mbele ya haki.

Sisi kama uongozi wa Wilaya tunatambua juhudi za mama mlezi wa kina Maria namna alivyohangaika kuwatunza na kuwalea hadi walipomaliza darasa la saba na kufaulu ktk shule ya msingi Ikonda.

Mama huyo yupo hapa Makete na tunamtambua kama MFIWA MKUU pamoja na wanamakete wote.

Wilaya itashiriki katika mazishi ya wapendwa wetu hao.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA.

Mbarikiwe wote.
Mwalemi๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo