ONYO Kali kutoka IKULU leo

Taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro sio za kweli na zipuuzwe.
Wananchi endeleeni kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya Serikali, na pia watumiaji wa mitandao ya kijamii mnakumbushwa kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria.
Serikali itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Novemba, 2017 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo