Uamuzi huo umefuatia baada ya taarifa ya chama cha msingi cha Milambo, iliyobainisha kuwa chama hicho kimemtumia mzabuni wa kusambaza pembejeo kampuni ya Petrobena East Africa ambayo haijaidhinishwa na serikali kuwa kampuni za usambazaji wa pembejeo nchini.
Kwa kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa Serikali pia imedhamilia kwa dhati kuhakikisha inatatua kero zinazowakabili wakulima.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry naye akaahidi kusimamia ili kuhakikisha wakulima hawanyonywi hasa katika kipindi cha masoko.
Joseph Kakunda ambaye ni mbunge wa jimbo la Sikonge, ameiomba serikali ilete wanunuzi zaidi wa zao la tumbaku ili kuongeza ushindani wa bei.
Katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa zao la tumbaku Waziri Tizeba ameagiza kutafutwa na kwa afisa wa bank wa NMB wilaya ya Urambo anayeshughulika na mikopo pamoja na mmiliki wa kampuni ya Petrobena East Africa aliyewarubuni wakulima ili waweze kuchukuliwa hatua.