Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aendelea Kukabwa Koo, Ni baada ya Kuagiza Vigogo washushwe Vyeo

DSCN0055Mtandao wa elimu Tanzania (TENMET) umemtaka mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, kufanya uchambuzi yakinifu kubaini changamoto halisi zinazoathiri ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi katika mkoa wake na kuzifanyia kazi.
Rai hiyo imetolewa katika tamko la mtandao huo kuhusu agizo la mkuu wa mkoa huyo kuvuliwa madaraka kwa walimu wakuu 63 wa shule za msingi na maafisa elimu wawili mkoani Mtwara kwa madai kutowajibika ipasavyo katika nyadhifa zao.
Akisoma tamkoa hilo la mtandao wa elimu Tanzania amesema tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa ufaulu wa wanafunzi unachangiwa na mambo mbalimbali yakiwemo ya upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, ukosefu wa mazingira rafiki shuleni, uwiano usio sahihi kati ya walimu na wanafunzi pamoja na ukosefu wa lishe bora, ambapo wamemtaka mkuu wa mkoa wa Mtwara kupata ushauri na maoni ya wadau muhimu wa sekta husika kabla ya kufanya maamuzi yenye athari kubwa kitaaluma na kijamii.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara alitoa uamuzi huo katika mkutano wa wadau wa elimu mkoa wa Mtwara, uliokuwa ukijadili changamoto zinazoikabili sekta ya elimu mkoani humo, ambapo katika kikao hicho ndipo mkuu wa mkoa alipotoa maamuzi hayo ambayo wadau wa elimu wamehoji kama kweli yatamaliza matatizo ya muda mrefu ya elimu mkoani humo.
Sambamba na hayo wadau hao wa elimu nchini wamesema hatua ya kuwavua madaraka baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi na maafisa wa elimu, na kuwateua wengine kujaza nafasi zao, kamwe halitaweza kuwa suluhisho la kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mkoa huo ambao hata hivyo katika matokeo ya kidato cha pili mwaka jana bado haijaweza kufanya vizuri.

Mtandao wa elimu Tanzania (TENMET) ni mtandao unaoundwa na Asasi 181 zisizo za kiserikali zinazojihusisha na masuala ya elimu, ambayo ilianzishwa ili kuhamasisha utolewaji wa elimu bora kwa usawa kwa kila Mtanzania.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo