skip to main |
skip to sidebar
Mwandishi wa habari wa Clouds TV apata ajali Mbaya
Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha CLOUDS TV mkoani Songwe, Ines Tobhias, amepata ajali na kuvunjika mguu wake huko katika eneo la Njelenje Mbeya Vijijini jana tarehe 31.08.2016, alipokuwa katika majukumu yake ya kikazi akitokea mjini Mbalizi akielekea wilaya ya Songwe (Mkwajuni) kwa usafiri wa Pikipiki.
Taarifa za awali zinasema kuwa pikipiki aliyokuwa akisafiria iligongwa na gari ndipo madhara hayo yakajitokeza.
Pichani hapo juu na chini akiwa amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika kwa ajili ya kumpokea Ines Thobias katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, akitokea katika Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Ifis Mbalizi Hospital.
Kushoto ni Thomson Mpanji akifuatiwa na Emmanuel Lengwa...
Mwandishi Ines Thobias, akishushwa kutoka katika gari la wagonjwa lililompeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Picha na Kenneth Ngelesi.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi