Hii ni Funga kazi, Wanaume 329,000 Mkoa wa Mbeya wafanyiwa tohara

JUMLA ya wanaume 329000, Kukoka Mkoa wa Mbeya wamefanyiwa tohara  katika kipindi cha miaka minne tangu 2012-2016, ikiwa ni sawa na asilimia 80 ya lengo walilowekewa na wazira ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.

Taarifa hiyo ilitolewa  hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa Dk Sefu Mhina wakati wa izunduzi wa Kondomu Mpya aina ya Zana ambayo inatolewa na serikali kwa kila mwanchi ikiwa ni jitihada za kupamba na maambuzki mapya ya VVU naUKIMWI nchni.

DK Mhina alisema kuwa tahara hiyo ni jitiada za Serikali za kupambana na maambuzui mapya hivyo kama Mkoa waliwekewa lengo la kuhakikisha wanapambana na moja ya njia ya kukabilina na maambukizi ni kuendesha tohara kwa wanaume.

‘Mbeya ni miongoni mwa yenye  maambuziki kwa kiwangom cha juu hivyo kuna njia mbalimbali za kupambana  na moja wapo ni kuendesha kampeni ya tohara kwa wanaume ambapo lengo likikuwa ifika mwaka  2017  tuwe tumesha tahiri wanaume 410,000  na mpaka sasa tayari wanaume 320,000 wamefanyiwa tohara aambpo ni sawa asilimia 80 ya lengo tuklilowekewa na wizara’ alisema Mhina.

Aidha Dk Mhina alisema njia nyingine walitumia kupambana na maambukizi mapya ni  upimaji wa afya kwa wajawazito ambapo katika kipindi cha Jenuari hadi Disemba 2015  wanawake 61,506 walipimwa huku 3,021 sawa na asilimia 4.9 walikutwa na maambukizi na kwamba wanaenndelea na kupata dawa lengo likiwa ni kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda mtoto.

Aidha Mhina alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia Jenuari- Jun mwaka 2016 jumla ya kondomu 6,000,000 za kiume na 30313 na kike zilisambazawa katika maneneo mbalimbali Mkoani hapa.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka UNAIDS Marie Engel alisema mbali na kupunguza kasi ya maambukizi lakini kondomu ya Zana ambayo itakuwa ikitolewa ,kaunzia ngazi ya serikali ya mtaa itapunguza mimba zisizo tarajiwa kwani tatizo hilo bado kwa nchi za Kiafrika bado ni kubwa.

Akizungumza katika uzinduzi wa kondomu ya Zana Kaimu Mkuu wa kitengo cha elimu habari na mawasiliano kutoka TACAIIDS, Eddah Charles alisema kuwa mpaka sasa jumla ya kondomu mil 21,000,000 zimetengenezwa kwa ajili ya kusambazwa nchini nzima huku Halmshauri ya jiji ikipewa kondomu 800,000 na Mbeya Vijijini kondomu 700,000.

Alisema sababu za Serikali kuzindua kondomu hiyo Mkoa wa Mbeya ni kutokana na Mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa mitatu amabyao maambukizi yake yapo juu kwa mujinu wa utafiti ulifanywa mwaka 2011 hadi 2015 ambapo mbeya ina asilmia 9 ikitanguliwa na Iringa yenye 9 pia huku Njombe ikiwa kinara kitaifa kwa kuwa na asilimia 14 ya maambukizi mapya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo