Wananchi wa mikoa ya Njombe na Mbeya hii leo wamejumuika pamoja na wageni waliotoka mataifa mbalimbali yakiwemo ya bara la ulaya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua ambalo katika kijiji cha litundu wilayani Wanging'ombe limeanza kujidhihirisha majira ya saa nne na dakika kumi mpaka saa tano na dakika 58
Baadhi ya waliofika katika kutazama tukio hilo wameonyesha furaha zao kwa kuwa hawakuweza kutazama mwaka 1979 na kwamba wanaamini kuwa awamu ijayo miaka 350 ijayo hawata kuwepo tena duniani wakati kwa upande wa wanafunzi tukio hili likiwa ni mafunzo kwa vitendo kwa kuwa wamekuwa wakisoma kwa nadharia
Issa Hamadi meneja wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kanda za nda za juu kusini anasema kwamba tukio la kupatwa kwa jua wameanza kulifuatilia tangu mwezi wa pili mwaka huu mara baada ya kampuni ya masuala ya anga ya nchi marekani kutangaza kuwa kupatwa kwa jua kutaonekana nchini Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi
Kampuni ya utalii ya UPL SAFARI kutoka jijini mbeya imefanikiwa kusafirisha watalii 36 kutoka mataifa mbalimbali na meneja wa kampuni hiyo Gabriel shawa akisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kulifuatilia tukio hilo kila mwaka ambapo hapo 2017 linataraji kutokea nchini marekani
Serikali mkoani Njombe inataraji kuweka alama ya ujenzi wa mnara na shule ya msingi katika eneo ambalo kupatwa kwa jua kumeonekana kwa asilimia 98 kijijini litundu wilayani wanging'ombe
Katika kipindi chote cha kupatwa kwa jua takribani saa moja hali ya hewa ilibadilika kuwa ya baridi sambamba na uwepo wa mawingu yalisababisha hali ya giza huku watazamaji wakiwa katika makundi kutizama jua kwa kutumia miwani maalumu iliyoletwa kutoka nchini nchini ujermani.
