Sakata la askari mgambo wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza kudaiwa
kufanya uharibifu wa mali za wafanyabiashara wa soko la matunda la
Kirumba jijini Mwanza usiku wa manane na kuwasababishia hasara ya kiasi
kikubwa cha fedha, hatimaye limechukua sura mpya baada ya Mbunge wa
jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na makazi Mh.
Angelina Mabula kuingilia kati kwa kuiamuru Manispaa hiyo kuwalipa fidia
ya hasara ya mali za wafanyabiashara hao.
Mabula anafika katika soko la Kirumba majira ya saa tano asubuhi na kulakiwa na vilio toka kwa baadhi ya akinamama wauza matunda.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Kirumba eEias Daud akatoa maelezo ya utangulizi kuhusiana na kilichojiri usiku wa manane ndani ya soko hilo.
Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kupitia kwa Mwenyekiti wake Nelson Mesha kimeendelea kulaani operesheni hiyo.

Kisha Mbunge wa Jimbo hilo la Ilemela Mh. Angelina Mabula akasimama kuongea na wajasiriamali hao akianza kwa kuwapa pole kutokana na kitendo kilichofanywa na askari mgambo nane.
Uharibifu huo wa matunda na mali nyingine za wafanyabiashara hao unaodaiwa kufanywa na askari mgambo wa Manispaa ya Ilemela majira ya saa tisa usiku wa manane wa kuamkia Ijumaa Agosti 26,umeathiri mitaji ya akinamama na vijana waliyoikopa katika taasisi za fedha na sasa hawajui ni nani atakayetegua kitendawili cha marejesho ya kila wiki ya mikopo hiyo kabla Manispaa ya Ilemela haijakamilisha kuwalipa fidia ya hasara ya mali zao.