Eneo la Mtaa wa Vikindu Mashariki mkoani Pwani kwenye nyumba ya
mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mzee Manitu paligeuka uwanja wa
mapambano baada ya polisi kuizingira nyumba hiyo na kupiga risasi nyingi
hewani wakati wakimtaka jambazi anayetuhumiwa kufanya mauaji ya katika
tukio la kuuawa askari polisi wanne waliokuwa wakibadilishana lindo
kwenye Benki ya CRDB Tawi la Mbande wilayani Temeke jijini Dar ajisalimishe.
Katika
tukio hilo Afisa wa Polisi mwenye cheo cha ASP Thomas Njuki wa Kikosi
Maalum cha Kupambana na Ujambazi inahisiwa ameuawa.
Baada ya jambazi huyo kumuua askari, jeshi la polisi liliongeza nguvu
eneo hilo na kupiga mabomu na risasi nyingi hewani zilisababisha
taharuki katika eneo hilo na kusababisha kila mmoja aseme lake.
Mapaparazi wetu baada ya kufika eneo hilo walitaka kuzungumzia na
maofisa wa polisi waliokuwa eneo hilo akiwemo, RPC wa Pwani, Bonaventura
Mushongi, Gilles na Kamishna Mwandamizi wa Jeshi hilo, Liberatus Sabas
lakini wote walisema hawawezi kuongea chochote mpaka wapate ruhusa
kutoka ngazi za juu kwa kuwa tukio hilo si la Kimkoa bali ni la Kitaifa.
Licha ya viongozi hao kukataa kuzungumza, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili ambaye alikuwa bega kwa bega na
askari hao alisema kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wanaume 7 ambapo
walikutwa wanaume 3 na wanawake 3 ambapo mwanaume mmoja aliyetajwa
kumuua Afisa huyo wa Polisi alitoroka pamoja na silaha yake.
HABARI: RICHARD BUKOS/ ISSA MNALLY /GPL.
