Mume amkata Panga Mkewe kisa kukutwa akizungumza faragha na mwalimu saa Nne Usiku

 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Dabil, Tarafa ya Bashnet wilayani Babati, Mkoa wa Manyara, Domitila Gabriel (25) amefariki dunia kwa kukatwa na panga na mumewe baada ya kukutwa akizungumza faragha na mwalimu mwenzake.
 
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Francis Massawe amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na chanzo chake kinadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Massawe siku ya tukio hilo, mwanaume huyo alimkuta mke wake akizungumza na mwalimu mwenzake wa kiume wakiwa peke yao wawili majira ya saa nne usiku, ndipo alipochukua uamuzi wa kumkata panga huku mwalimu mwenzake akikimbia kuepuka kuuawa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo