NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, amewaasa
wasimamizi wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi hiyo
kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na
uelewa kufaulu mtihani huo.
Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojuka kusoma na
kuandika kufaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi
hao kushindwa kunyakazi hiyo kwa makini.
Chongolo aliyasema hayo jana, wakati akizindua semina ya
mafunzo kwa wasimamizi hao wilayani Londogo ambapo alisema usimamizi
hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo
kitaaluma.
Alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua
kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa
msimamizi wa mtihani.
“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha
wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mtihani huo, kufanya hivyo ni
kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani,” alisisitiza.
Hivyo aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika
kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu
kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.
Alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma,
uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia
mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.
Aliongeza kuwa mitihani huo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini.
