Anyakuliwa na mamba ziwani akivua samaki

Mkazi wa Kijiji cha Kakobe, Kata ya Kazunzu katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Mkoa Mwanza, Juma Abdallah (30) anadaiwa kuliwa na mamba na mabaki ya mwili wake bado hayajapatikana.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kazunzu, Thimothy Chuma alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Agosti 25 baada ya Abdallah akiwa na Hamisi Magayane wakivua samaki kandokando ya Ziwa Victoria kurukiwa na mamba huyo na kutokomea naye.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka Magayane (23), walipiga filimbi na wananchi kukusanyika kuanza kumsaka mamba huyo, lakini hakupatikana.

Diwani wa Kata ya Kazunzu Boniphace Msenyela aliwasihi wananchi kuendelea kumsaka mamba huyo, kwani anapopata chakula hujificha katika miamba.

Msenyela alisema anaendelea kuwasiliana na maofisa wanyamapori ili kusaidia kumsaka mamba huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo