Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa wasaidizi wa kisheria wilaya ya Makete MADIPASE Mch.Denis Sinene ofisini kwake ambapo akitoa taarifa ya mashauri waliyopokea kwenye mamalaka ya mji mdogo wa Iwawa pekee kwa ajili ya kutoa elimu kutoka kwa wananchi suala la ardhi limechukua idadi kubwa kuliko maswala Ya ndoa, mirathi, mambo ya watoto na madai mengineKutokana na kufanikiwa kuwasaidia, kuwaelimisha na kusuluhisha mashauri mbalimbali watu wengi mwenyekiti huyo amewataka wananchi kutumia huduma hiyo bure kwa kwenda katika ofisi zao ama kupiga simu ambazo wamekuwa wakizitaja katika vipindi vya mwanansheria wetu vinavyorushwa na redio Green FmMch.Sinene hakuacha kutoa wito kwa wananchi juu ya msaada huo wa kisheria wanaoutoa kwa jamiiIkumbukwe kuwa wasaidizi wa msaada wa kisheria wilaya ya Makete wapo katika kata zote za wilaya hiyo
Na Henrick Idawa