Kilichojiri Siku ya wauguzi Duniani, Mkoa wa Njombe imefanyikia Makete

Wauguzi mkoani Njombe Wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja licha ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa kuwa serikali inazitambua na inaendelea kupambana nazo

Hayo yamesemwa na mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Francis Namaumbo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani iliyofanyika leo kimkoa wilayani Makete mkoani Njombe

Bw Namaumbo amesema ni kweli sekta ya afya inachangamoto mbalimbali na pia serikali haijakaa kimya imekuwa ikizitatua kwa kadri ya uwezo wake hiyo wauguzi wasikate tamaa bali waendelee kufanya kazi zao kwa moyo kwa kuwa wao ni watu muhimu katika ujenzi wa taifa

Awali Bw. Clarance Mandawa akisoma Risala ya wauguzi kwa mgeni Rasmi, hakusita kutaja mafanikio yaliyofanywa na wauguzi wa mkoa wa Njombe ikiwemo kupunguza idadi ya vifo vya kina mama vinayotokana na uzazi kutoka kina mama 91 kati ya laki moja mwaka 2014 hadi kufikia 90.8 kati ya laki moja wanaojifungua mwaka 2015
Pia katika risala hiyo hawakusita kutoa changamoto zinazowakabili wauguzi hao ikiwa ni pamoja na kucheleweshwa kupandishwa vyeo, kutolipwa fedha za likizo kwa wakati pamoja na kucheleweshwa kubadilishwa vyeo baada ya kurudi masomoni

Katika maadhimisho hayo Afisa Utumishi na utawala wilaya ya Makete Bw. Nicodemus Tindwa amepewa nafasi ya kujibu changamoto zilizojitokeza

Siku ya wauguzi duniani huadhimishwa Mei 12 ya kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni "WAUGUZI NGUVU YA MABADILIKO YA UBORESHAJI THABITI WA MIFUMO YA AFYA"


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo