Wakulimawalambwa bakora za kutosha Morogoro

Wananchi wa kijiji cha Tindiga wilayani Kilosa mkoani Morogoro wamelalamikia kuchapwa viboko na wafugaji jamii ya wamasai ambapo wamesema wanawavamia mashambani na kulisha mifugo yao kwa nguvu mazao ya wakulima kutokana na uhasama uliopo baina ya pande hizo mbili.

Wakizungumza mbele ya mbunge wa jimbo la mikumi Bw.Joseph Haule alipotembelea kijijini hapo wananchi wa kijiji cha Tindiga wamesema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu na kwamba serikali ya wilaya ya Kilosa wameshindwa kuushughulikia mgogoro huo  hali inayosababisha uhasama unaopelekea wafugaji kuwachapa viboko wakulima wakiwemo watoto wanapoenda kuchota maji. 
 
Naye mmoja wa wafugaji wa kijiji cha Tindiga Bw.Kalaita Motosio amesema kushamiri kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji inayo pelekea kutoelewana inasababishwa  na viongozi wa ngazi mbalimbali wanaogawa maeneo ya ardhi bila kufuata taratibu.
 
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu Prof J ameahidi kushughulikia kero hiyo na kuwashutumu viongozi wa vijiji kutokana na kudaiwa kujihusisha na mazingira ya rushwa na kusababisha kero hiyo ambayo ni ya muda mrefu huku akiwashauri wananchi kufikisha malalamiko yao kwa viongozi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo