Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya saa mbili na nusu usiku wakati mtia nia huyo alipokuwa matembezini kuelekea nyumbani kwake.
Baadhi ya mashuhuda waliomsaidia mtu huyo walisema walisikia kelele zikipigwa akiomba msaada na mara baada ya kufika walikuta mtu mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala sura yake akiwa anatokomea.
“Mimi nilifika hapa kumpa msaada huyu kama jirani yangu nilisikia akipiga kelele nilifika na kuona mtua akiwa ameshika panga na anaishilizia gizani kwahiyo sikuweza kumfahamu”alisema shuhuda wa tukio hilo.
Mke wa mtia nia huyo Sara Mtalima alisema kuwa mme wake hakuwa na ugomvi na mtu yeyote lakini tangu atangaze nia kupitia Chadema amekuwa akipewa vitisho kupitia simu yake ya mkononi.
“Mme wangu hajawahi kugombana na mtu yeyote yule na hapa kijijini anaelewana na kila mtu, lakini tangu atangaze nia amekuwa akitishiwa kweye simu yake hali iliyomsababisha mpaka kuogopa kutembea”,alisema Sara.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita Adam Sijaona walimpokea majeruhi huyo na kumlaza katika wodi Namba 8 na kwamba hali yake inaleta matumaini kidogo kutokana na kukatwa mapanga mengi kichwani na kuvuja damu nyingi.
Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi Peter Kakamba alipotafutwa kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.
Na Valence Robert- Malunde1 blog Geita