Jeshi la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini humo.
Hata hivyo taarifa za jeshi hilo zinasema kuwa kiongozi wa kituo hicho cha Boko Haram Babuji Ya'ari amekamatwa.
Ya'ari pamoja na kutuhumiwa kuhusika katika
utekaji wa wasichana hao lakini pia alihusika katika mauaji ya kiongozi
wa kijadi wa Gwoza, imebainisha taarifa ya serikali.
Jeshi hilo pia limegundua kuwa Ya'ari aliyekuwa
mfanya biashara alikuwa akijifanya ni mwanaharakati katika kutokomeza
kundi la Boko Haram ili kupata nafasi ya kuchunguza harakati za jeshi la
Nigeria na mipango dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Anatuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya
mashambulio kadhaa likiwemo lile lililotokea Maiduguri na makao makuu ya
mji wa Borno mwaka 2011