Daktari wa meno aliyejulikana kwa jina la Dokta Ngariba (54),
amejikuta ndani ya janga la tuhuma za ngono baada ya wapiga picha za Udaku kunasa sakata lake na mwanamke aliyedai ni
mgonjwa wa jino aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamida (20).
Tukio hilo la kushangaza lilijiri Juni 9, mwaka huu ndani ya Kituo
cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kilichopo Kigamboni jijini
Dar ambapo timbwili hilo lilitokea.
Ilikuwa
wakati mwandishi akizunguka katika Jiji la Dar es
Salaam kusaka matukio ndipo alipopita nje ya kituo hicho alisikia
sekeseke kutokea kwenye chumba ambacho baadaye kilibainika na
cha kung’olea meno.
Katika uchunguzi na ufuatiliaji ,
mgonjwa huyo alisikika akidai kwa polisi waliofika kutuliza sakata kuwa,
alijihimu kwenye kituo hicho kwa lengo la kung’oa jino lakini katika
hali ambayo hakuitarajia daktari huyo alimtaka kimapenzi naye akajikuta
akitumbukia.
“Mimi nimekuja kung’oa jino, linaniuma leo sijui
siku ya ngapi? Lakini huyu daktari nimefika akanitaka kimapenzi.
Nilidhani anatania, baadaye nikagundua kuwa amedhamiria,” alisema
mwanamke huyo ambaye alikutwa ameshavua dera.
Hata hivyo, daktari huyo hakumwacha mgonjwa
wake huyo atambe kiasi hicho, alijibu mapigo kwa kusema kuwa, alimpokea
mwanamke huyo kama mgonjwa wa jino na kumwingiza kwenye chumba cha
kung’olea meno lakini ghafla alimwona akianza kuvua nguo zake kisha
kumvua na yeye shati na baadaye kutaka kufungua zipu ya suruali.
Akiendelea kuzungumza mbele ya Polisi wa Kituo cha Kigamboni
waliofika kwenye sakata hilo ndani ya chumba cha matibabu ya meno,
daktari huyo alisema:
“Mimi sikuwa na nia mbaya, nilijua ni mgonjwa anataka tiba ya kung’olewa jino.
“Sasa nikiwa katika maandalizi ghafla nikamwona anavua nguo na kisha
akanivaa mimi na kuanza kunivua shati. Nashangaa sana anaposema
nilimtaka kimapenzi, si kweli jamani.”
Baada
ya maelezo ya Dokta Ngariba, mwandishi alikuwa na maswali yake lakini
hakupewa nafasi ya kuyauliza kwa vile alidandia ugomvi.
Swali la kwanza; kama kweli Dokta Ngariba alivamiwa na kuvuliwa nguo
na mgonjwa huyo, alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa watumishi
wenzake?
Swali la pili; mpaka mgonjwa anajivua nguo zake kisha
kumvua yeye shati na baadaye kuelekea kwenye fraizi ya suruali, yeye
alikuwa anawaza nini akizingatia ni mgonjwa wa meno?
Wakielekea kituo cha Polisi Kigamboni.
Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:
Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:
“Taarifa hizo nazisikia kwako, niko safarini, nitafuatilia. Kama ni
kweli hatua zinachukuliwa kwa waajiri wake ambapo najua kwa kosa kama
hilo ni kupoteza kazi.”
Chanzo: Gazeti la Uwazi/Gpl
Chanzo: Gazeti la Uwazi/Gpl