![]() |
Mkaa huu unauzwa sh. 8000/= kutoka 5000/= ya awali |
Bei ya mkaa wilayani Makete inazidi kupanda siku hadi siku
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo
Kupanda mara kwa mara kwa bei hizo kumesababishwa na mvua
zinazoendelea kunyesha wilayani humo hivyo kupelekea ugumu wa kutengeneza mkaa
hivyo wengi wa waandaaji wa mkaa kuacha
Mmoja wa muuzaji mkaa aliyejitambulisha kwa jina la Tweve
amesema idadi ya waliokuwa wakiandaa mkaa kutoka kwenye kijiji chake cha
Ivalalila wameacha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo
“Unajua uchomaji wa mkaa unakuwa mgumu sana kipindi hiki,
ukianda magogo kwa ajili ya kuyachoma ili upatikane mkaa, mvua inayesha na moto
unazima, kwa hiyo sisi tunaojitahidi hivyo hivyo inatulazimu kupandisha bei”
alisema Tweve
Bei ya gunia la mkaa hivi sasa imepanda kutoka sh. 8000/=
ambapo hivi sasa gunia linauzwa kati ya shilingi 10,000 hadi 15,000/= jambo
linalowapa tabu watumiaji wa mkaa huo
Hata hivyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani
Makete zinapelekea wananchi wengi kutumia zaidi mkaa kuliko kuni kutokana na
kuni hizo kulowa, lakini bidhaa hiyo ya mkaa nayo inazidi kupungua kutokana na
wauzaji kuwa wachache