Hili si zizi la Mbuzi au banda la
kuku bali ni Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyopo Kijiji cha Kyaseni Kata ya Uru Mashariki, Wilaya
ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro. Ofisi hii
iliyopo katika jimbo la Mbunge Thirili Chami ni miongoni tu mwa ofisi
nyingi za chama hicho katika vijiji vingi nchini ambazo zipo katika hali mbaya huku baadhi ya Vijiji Kama kile cha Kipera,
Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani
Mvomero Mkoani Morogoro vikiwa havina kabisa Majengo ya Ofisi za chama hicho
Tawala jambo ambalo linaathiri utendaji wa Viongozi wa Chama ambao ndio
wameshikilia mhimili wa kuiongoza dola.Picha na Father Kidevu